Jeshi la Ulinzi la Taifa la Burundi (FDNB), limetangaza kuwa limepata wanajeshi wapya waliokamilisha mafunzo ya upelelezi.
Alhamisi, tarehe 5 Juni, maafisa hao wa ujasusi walihitimisha mafunzo ya miezi sita yaliyofanyika Kinanira.
Kupitia ukurasa wake rasmi wa X (zamani Twitter), FDNB ilisema kuwa maafisa hao waliagizwa “kutumia ujuzi waliopata kwa manufaa ya nchi.”
Wamo pia wanawake waliopata mafunzo hayo ya kijasusi.
Hata hivyo, baada ya kumaliza mafunzo yao, Burundi ilikosolewa na kudhihakiwa kwa kuchapisha picha za maafisa wake wa ujasusi, licha ya kuwa kazi yao inapaswa kufanywa kwa siri.

Zaidi ya wapelelezi 30 wameongezwa katika safu za jeshi la Burundi.
Wapelelezi hao, wakiwemo wanawake, walipokea vyeti baada ya kuhitimu.



