President_Donald_Trump_shakes_hands_with_Rwandan_President_Paul_Kagame

Trump: Nistahili Tuzo ya Amani ya Nobel kwa Kazi Yangu Rwanda na DRC

Sangiza iyi nkuru

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump amesema anastahili Tuzo ya Amani ya Nobel kutokana na juhudi zake katika kutatua migogoro kati ya mataifa kama vile Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Rwanda na DRC zimekuwa zikifanya mazungumzo chini ya upatanisho wa Marekani, ili kumaliza mzozo uliodumu kwa miaka mitatu kati ya mataifa hayo jirani.

Mzozo huo unasababishwa na mapigano kati ya jeshi la serikali ya Kinshasa na kundi la waasi la M23, ambalo DRC inadai linaungwa mkono na Rwanda.

Kupitia mtandao wake wa kijamii wa Truth Social, Trump alisema kuwa yeye na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio walifanikiwa kufikia makubaliano ya amani kati ya Rwanda na DRC.

Alisema:

“Ninafuraha kutangaza kuwa mimi na Waziri wa Mambo ya Nje Marco Rubio tumefanikisha makubaliano bora ya amani kati ya Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, katika vita vilivyosababisha umwagaji mkubwa wa damu na vifo zaidi ya migogoro mingine mingi ya miaka mingi iliyopita.”

Trump alisema kuwa makubaliano hayo yatatiwa saini na wawakilishi wa Rwanda na DRC siku ya Jumatatu, tarehe 23 Juni, kinyume na taarifa za awali za Washington zilizotaja tarehe 27 Juni.

Katika mahojiano na Fox News, Trump alidai kwamba kazi aliyofanya kwa ajili ya Rwanda, DRC, na nchi nyingine nyingi inampa nafasi ya kushinda Tuzo ya Amani ya Nobel ya mwaka 2026.

Alisema:

“Wanipashe tuzo ya Nobel kwa nilichokifanya Rwanda, Kongo, Serbia, Kosovo… ni maeneo mengi. Ila kubwa zaidi ni kazi niliyofanya India na Pakistan. Kusema kweli, ningepewa tuzo hiyo mara nne au tano.”

Trump pia alikiri kupitia Truth Social kuwa anafahamu hatapokea tuzo hiyo licha ya kustahili.

Akizungumzia tena makubaliano ya Rwanda na DRC alisema:

“Huu ni siku muhimu kwa Afrika, na kwa hakika kwa dunia nzima. Lakini sitapewa Tuzo ya Amani ya Nobel kwa hili. Siwezi kupewa tuzo kwa kusitisha vita kati ya India na Pakistan, wala kati ya Serbia na Kosovo, wala kwa kusaidia kudumisha amani kati ya Misri na Ethiopia—licha ya msaada mkubwa wa Marekani.”

Trump alikumbusha pia kuhusu Makubaliano ya Abraham kati ya Israel na nchi kadhaa za Mashariki ya Kati kama sababu nyingine inayomfanya astahili tuzo hiyo.

Akaongeza:

“La hasha, sitapewa tuzo ya Nobel—haijalishi nifanye nini, hata kazi yangu kuhusu Ukraine na Urusi, au Israel na Iran. Matokeo yawepo, lakini watu wafahamu haya ndio mambo muhimu kwangu.”

Pakistan ndiyo iliwasilisha jina la Trump kwa Tuzo ya Amani ya Nobel, baada ya kusaidia kusitisha vita kati ya nchi hiyo na India juu ya mgogoro wa Kashmir.

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *