5e1u8hpk_us-iran-israel-afp_625x300_12_June_25

Iran Kufanana na Japan? Marekani Yatishia Mashambulizi ya Kinyuklia

Sangiza iyi nkuru

Wakati vita kati ya Israel na Iran vikizidi kuongezeka, kuna wasiwasi kuwa Marekani huenda ikaingia vitani, hali ambayo inaweza kuleta madhara makubwa kwa Iran, na kuifanya ifanane na Japan ya mwaka 1945.

Rais Donald Trump hivi karibuni alitangaza kuwa amejiwekea muda wa wiki mbili ili kufanya uamuzi kuhusu kushambulia Iran kwa lengo la kuzuia mpango wake wa nyuklia.

Baadhi ya wachambuzi wanasema kuwa iwapo Marekani itashambulia Iran, huenda ikatumia nguvu za kijeshi sawa na zile zilizotumika Hiroshima na Nagasaki, ambapo Japan ilishambuliwa kwa mabomu ya kinyuklia na vita vya pili vya dunia vikafikia tamati.

Kauli hii imezua mjadala mkali katika ulingo wa kimataifa. Urusi imeonya Marekani kuwa shambulizi ambalo lingemuua kiongozi mkuu wa Iran au kuliharibu jeshi la taifa hilo kabisa “litafungua sanduku la Pandora”, likimaanisha kuanzisha vita vikubwa vya kikanda.

Iran nayo imesisitiza haitakubali mazungumzo yoyote na Marekani mradi tu Israel inaendelea na mashambulizi. Kwa upande mwingine, mataifa ya Ulaya yanajitahidi kutafuta suluhu kwa njia ya mazungumzo yanayoendelea huko Geneva.

Wachambuzi wanaonya kuwa iwapo Marekani itatumia silaha za kinyuklia dhidi ya Iran, taifa hilo linaweza kutumbukia gizani kama ilivyotokea kwa Japan baada ya Vita vya Pili vya Dunia. Hata hivyo, baadhi ya watu wanaona hii ni mbinu ya Trump kuishinikiza Iran ikubali mazungumzo, huku wengine wakihofia kuzuka kwa mzozo wa kimataifa.

Ni suala la muda tu kabla ya kujua kama kauli hizi ni mbinu za shinikizo au ni mwanzo wa tukio litakaloiweka Iran katika hali sawa na Japan iliyoharibiwa na mabomu ya kinyuklia.

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *