Kocha wa PSG akamatwa katika uchunguzi wa ubaguzi

Sangiza iyi nkuru

Kocha wa Paris Saint Germain, Christophe Galtier, alishikiliwa kwa mahojiano pamoja na mwanawe kama sehemu ya uchunguzi wa madai ya ubaguzi, mwendesha mashtaka wa Nice aliambia AFP siku ya Ijumaa .

Hatua hiyo inafuatia uchunguzi ulioanzishwa mwezi Aprili, kufuatia madai kwamba alitoa matamshi ya ubaguzi wa rangi na chuki dhidi ya Uislamu kuhusu wachezaji alipokuwa akiifundisha Nice msimu wa 2021/22.

Mwendesha mashtaka alisema watatoa taarifa zaidi kuhusu kukamatwa kwa Galtier na mwanawe John Valovic-Galtier, wakala wa mchezaji, kupitia taarifa baadaye Ijumaa.

Galtier anatazamiwa kutimuliwa na wamiliki wa PSG wa Qatar baada ya msimu ambao haukuwa na matokeo mazuri ambapo PSG ilipokea vipigo 10 mnamo 2023, na kuondoka kwenye Ligi ya Mabingwa, lengo kuu la timu hiyo, katika hatua ya 16 bora.

Madai hayo yaliibuka kwa mara ya kwanza kwenye vyombo vya habari vya Ufaransa mwezi Aprili.

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *