Mkuu wa Jeshi la Ulinzi ya Kenya (KDF), Jenerali Francis Ogolla amefanya ziara nchini Rwanda, Jumanne Juni 27, 2027, ambapo alipokelewa na kufanya mazungumzo na mwenzake wa Rwanda, Luteni Jenerali Mubarakh Muganga.
Wizara ya Ulinzi nchini Rwanda imetangaza kuwa mazungumzo kati ya Wakuu wa Ulinzi yalilenga ushirikiano katika kudumisha usalama katika eneo hilo, pamoja na kupanua ushirikiano uliopo.
Katika makao makuu ya Jeshi la Rwanda, Kimihurura, Jen. Francis Ogolla alipokelewa kwa heshima na mwenzake Mkuu wa Majeshi Lt Jen Mbarakh Muganga. Jenerali Francis Ogolla, alikutana na Waziri wa Ulinzi wa Rwanda, Marizamunda Juvenal
Jenerali Francis Ogolla amefanya ziara ya siku mbili nchini Rwanda, ambako amehudhuria kuhitimishwa kwa zoezi la kudumisha na kurejesha amani, linalounganisha Majeshi ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayojulikana kwa jina la ’Ushilikiano Imara’.
Alisema baada ya kushiriki kuhitimisha zoezi la Ushirikiano Endelevu katika Wilaya ya Musanze, ilimlazimu kufanya mazungumzo na wenzake wa Rwanda.
Katika siku ya mwisho ya ziara yake nchini Rwanda, Gen. Ogolla, Jumanne asubuhi, pia alitembelea tovuti ya kumbukumbu ya Mauaji ya Kimbari ya Kigali, ambapo alionyeshwa sehemu na kuelezea historia iliyosababisha Rwanda kwenye mauaji ya halaiki, na kuweka maua kwenye makaburi ambayo zaidi ya miili 250 elfu ilizikwa.
Kwa zaidi ya miaka 20, Rwanda na Kenya zimekuwa na ushirikiano wa karibu wa kijeshi, ikiwa ni pamoja na uhamisho wa ujuzi katika kozi za kijeshi, pamoja na ushirikiano katika shughuli za pamoja za kijeshi kati ya nchi hizo mbili.
Bagabo John


