Serikali ya Uingereza itataka kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama kwamba mpango wake wa kuwafukuza makumi ya maelfu ya watu wanaotafuta hifadhi nchini Rwanda ulikuwa kinyume cha sheria, Waziri Mkuu Rishi Sunak alisema Alhamisi .
Mahakama ya Rufaa ilihitimisha kwamba Rwanda isingeweza kuchukuliwa kama nchi ya tatu salama.
“Ingawa ninaheshimu mahakama kimsingi sikubaliani na maamuzi yao,” Sunak alisema katika taarifa.
“Rwanda ni nchi salama … Sasa tutaomba kibali cha kukata rufaa dhidi ya uamuzi huu katika Mahakama ya Juu.”


