Makaburi 40 mapya ya halaiki yamegunduliwa katika msitu mkubwa wa Shakahola, nchini kenya, huku awamu ya nne ya zoezi la uchimbaji ikirejea Jumatatu .
Waziri wa Usalama wa Ndani Kithire Kindiki alisema makaburi 40 ambayo bado hayajafukuliwa yanashukiwa kuwa na miili mingi.
Kindiki aliendelea kusisitiza dhamira ya serikali ya kukabiliana na wahubiri wahuni.
Akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa afisi ya Naibu Kamishna wa Kaunti katika kaunti ndogo ya Igoji katika kaunti ya Meru, Kindiki alisema mpango huo unalenga kuhakikisha hakuna Mkenya mwingine atakayekumbwa na mkasa mwingine kama wa Shakahola.
Idadi ya vifo kutokana na mkasa huo sasa imefikia 339 hadi sasa.
Miili ya wafuasi wa Pastor Mackenzie’s Goodnews International Ministries imepatikana kwenye makaburi ya kina kirefu msituni katika kile kinachochunguzwa kama mauaji ya halaiki.
Mackenzie ameshutumiwa kwa kuwahangaisha waathiriwa hadi kufa kwa njaa kwa kuamini kwamba wangekutana na Yesu Kristo.
Source: The Star Kenya


