Wawakilishi wa RPF Inkotanyi wamemaliza ziara yao nchini Tanzania

Sangiza iyi nkuru

Ujumbe wa RPF Inkotanyi ukiongozwa na Katibu Mkuu Wellars Gasamagera, umemaliza ziara ya siku nne nchini Tanzania, ambapo ulifanya mazungumzo na Chama Cha Mapinduzi (CCM), chama tawala.

Ni ziara ambayo ujumbe huo ulianza kuanzia Juni 30 hadi Julai 5, 2023. Katika ziara hiyo Katibu Mkuu wa RPF Inkotanyi Gasamagera amefanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa chama tawala nchini Tanzania (Chama cha Mapinduzi/CCM) Daniel Chongolo. Katika mijadala hiyo, pande zote mbili zilikubaliana kuendeleza mahusiano kwa kuzingatia uwezo wa pamoja hasa kwa nchi hizo mbili.

Wawakilishi hao wa Chama cya FPR Inkotanyi walitembelea miradi mbalimbali ya CCM, ikiwemo Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere iliyopo Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani nchini Tanzania.

Bagabo John

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *