unnamed

Nigeria: Mapigano Makali Kati ya Wakulima na Wafugaji Yaua Watu 56 Benue

Sangiza iyi nkuru

Watu wasiopungua 56 wameuawa wiki hii kufuatia mashambulizi mawili ya kihalifu yanayodaiwa kufanywa na wafugaji wa kuhamahama katika jimbo la Benue, katikati mwa Nigeria.

Awali, ofisi ya gavana ilikuwa imetangaza vifo 17 pekee, lakini idadi hiyo imesasishwa rasmi Jumamosi, kwa mujibu wa ripoti ya Al Jazeera.

Msemaji wa serikali alisema idadi ya vifo huenda ikaongezeka zaidi, kutokana na juhudi zinazoendelea za uokoaji na uchunguzi.

Ijumaa, msemaji wa polisi, Anene Sewuese Catherine, alieleza kuwa “idadi kubwa ya washambuliaji waliokuwa na silaha walivamia eneo hilo usiku kucha”.

Mashambulizi haya ni sehemu ya mzozo wa muda mrefu kati ya wakulima na wafugaji unaoendelea kugharimu maisha ya mamia ya watu nchini Nigeria.

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *