21-photo_9-2e93c

Wakazi wa Goma Waonywa Kuhusu Mabomu Hatari Yaliyosalia

Sangiza iyi nkuru

Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC) imetoa onyo kuhusu uwepo mkubwa wa mabomu yaliyosalia bila kulipuka katika maeneo mbalimbali ya jimbo la Kivu Kaskazini.

Destin Nalanda, mtaalamu kutoka ICRC anayefuatilia athari za silaha kwa raia wanaoishi karibu na maeneo yenye mizozo, alisema kuwa baadhi ya maeneo ya jiji la Goma yamejaa mabomu hatari.

Nalanda alieleza kuwa mabomu hayo ni mabaki ya mapigano yaliyotokea mwanzoni mwa mwaka huu ambapo waasi wa M23 walitwaa mji wa Goma, na kuwafurusha wanajeshi wa serikali ya DRC.

Kulingana naye, kati ya Januari na Machi mwaka huu, zaidi ya watu 300 walijeruhiwa na mabomu yaliyotupwa na pande zilizozozana.

Watu hao walikuwa miongoni mwa zaidi ya 1,000 walioumia kwa silaha na kutibiwa katika Hospitali ya CBCA Ndosho katika kipindi hicho.

ICRC imewaonya wakaazi wa mashariki mwa DRC kuwa waangalifu na kutoigusa vitu visivyojulikana, kwani vinaweza kuwa mabomu hatari.

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *