Msemaji wa Chuo Kikuu cha Rwanda (UR), Kabagambe Ignatius, amemkosoa mtu anayetumia jina la Keza Leila kwenye mtandao wa X, ambaye hivi karibuni alidai kuwa wahadhiri wa chuo hicho huwatishia wanafunzi wa kike kuwafeli mitihani iwapo watakataa kufanya nao ngono. Kabagambe alisema kuwa hakuna mwanafunzi mwenye jina hilo au taarifa hizo anayesoma katika chuo hicho.
Mnamo Novemba 11, 2026, mtu huyo aliyejitambulisha kama Leila alichapisha ujumbe kwenye X akidai kuwa rushwa ya ngono imekithiri miongoni mwa wahadhiri na viongozi wa Chuo Kikuu cha Rwanda.
Mnamo Novemba 12, 2026, Kabagambe alisema kuwa mtu anayetumia jina la Leila kwenye X alikuwa akisambaza taarifa zisizo za kweli. Aliongeza kuwa chuo hicho hakina mwanafunzi anayeitwa Keza Leila.
Kabagambe alisema: "Acha kuendelea kusambaza madai yako ya kupita kiasi na yenye lengo la kuchafua watu kupitia akaunti yako bandia (catfish). Wewe si mwanafunzi anayefahamika katika Chuo Kikuu cha Rwanda (UR). Hatukujui kwa sababu jina la Keza Leila halionekani popote katika kumbukumbu zetu."
Hii ni baada ya Kabagambe kuchapisha ujumbe mwingine kwenye X akimwambia Leila kuwa alikuwa "anatafuta tu wafuasi kwenye X, na sasa anawapata."
Kwa upande wake, Leila alisema: "Tulidhani kwamba tulikuwa na msemaji ambaye alipaswa kutuwakilisha, kuwasilisha matatizo yetu na kuhakikisha kuwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Rwanda wanasikilizwa. Lakini hili ni jambo la kukatisha tamaa!"
Wawili hao wameendelea kujibizana kupitia X, huku Ofisi ya Upelelezi ya Rwanda (RIB) ikimwomba Leila kuwasilisha maelezo zaidi ili iweze kufanya uchunguzi wake.
Hii si mara ya kwanza kwa madai ya rushwa ya ngono, inayojulikana pia kama "ngono ili upewe alama za mitihani", kuvugwa katika Chuo Kikuu cha Rwanda. Baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii pia wamekomentari kuwa wanafahamu kuwepo kwa vitendo hivyo katika chuo hicho.

