a126d390-50be-11f0-a136-53d7f1f40c12.jpg

Jessie J Afanyiwa Upasuaji wa Matiti Kufuatia Ugonjwa wa Saratani

Sangiza iyi nkuru

Mwanamuziki wa Uingereza, Jessie J, ametangaza kuwa amefanyiwa upasuaji wa matiti baada ya kugundulika kuwa na saratani. Msanii huyo mwenye umri wa miaka 37 amesema kwa sasa yuko nyumbani akipumzika akisubiri majibu ya upasuaji huo.

Kupitia mitandao ya kijamii, Jessie J aliwashukuru madaktari na wauguzi waliomhudumia, na akashiriki picha na video zinazoonyesha alivyotumia siku mbili zilizopita — ikiwemo video inayomuonesha akiimba akiwa hospitalini akisubiri kupelekwa chumba cha upasuaji.

Mwanzoni mwa mwezi Juni, alitangaza hadharani kuhusu kugundulika na saratani ya matiti, hatua iliyopokelewa kwa pongezi nyingi kutoka kwa watu waliothamini ujasiri wake na nia ya kusaidia wengine wanaopitia hali kama yake.

Pia alielezea shukrani kwa familia yake na mashabiki kwa kuwa naye bega kwa bega, na kutoa ujumbe wa faraja kwa wale walioko kwenye safari kama yake: “Tutaweza, nawajali nyote.”

Mashabiki wake na marafiki zake wa tasnia ya muziki walimtumia salamu za faraja na kumtakia uponyaji wa haraka, wakimwita shujaa wa kweli.

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *