téléchargement

Msichana Aliyedaiwa Kulenga Viongozi wa Twirwaneho Aachiwa Huru Baada ya Siku Mbili

Sangiza iyi nkuru

Msichana mmoja anayeitwa Nyamanoro, kutoka Ndondo ya Bijombo, aliyekamatwa hivi karibuni kwa tuhuma za kupanga njama ya kuwaua viongozi wa kundi la Twirwaneho kwa ujanja, ameachiwa huru.

Nyamanoro aliachiwa kwa msamaha siku ya Ijumaa tarehe 29, baada ya kuzuiliwa kwa siku mbili katika eneo la Mikenke, alikokuwa amepelekwa baada ya kukamatwa akitokea Ndondo ya Bijombo. Inasemekana alikuwa ametumwa na watu wa karibu na serikali ya Rais Félix Tshisekedi kutafuta nambari za simu za baadhi ya viongozi wa Twirwaneho huko Minembwe, hasa za Brigedia Jenerali Sematama, anayejulikana kama Intare-Batinya.

Ripoti zingine zinadai kuwa alihaidiwa zawadi au malipo kwa kazi hiyo, ingawa haikuelezwa ni zawadi ya aina gani. Kuachiwa kwake kumezua mijadala, wengine wakisema uchunguzi ulithibitisha hana hatia, lakini wengine wakidai kuwa viongozi wa Twirwaneho walimsamehe.

Nyamanoro anatokea Kajembwe, katika grupema ya Bijombo, wilaya ya Uvira—eneo linalodhibitiwa na kundi la waasi la Gumino, linaloongozwa na Nyamusaraba, ambalo linashirikiana na serikali ya Kinshasa. Eneo hili pia linadhibitiwa na majeshi ya FARDC (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo) pamoja na FDNB (Jeshi la Burundi).

Wakati wa kukamatwa kwake, inasemekana alikuwa na mawasiliano ya wanachama wa Gumino, jambo lililothibitisha uwepo wa ushirikiano kati yake na Gumino, na kuonyesha kuwa serikali ya Kinshasa huenda ilimtumia kwa kazi hiyo.

Serikali ya Kinshasa inasemekana ilikuwa ikitafuta nambari za simu za viongozi wa Twirwaneho kwa lengo la kuwashambulia kupitia ndege zisizo na rubani (drones), kama ilivyotokea mwezi wa pili mwaka huu wakati Michel Rukunda Makanika, aliyekuwa kiongozi mkuu wa Twirwaneho, aliuawa kwa shambulio la drone.

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *