shutterstock-editorial-15387215h

Nyimbo Mpya za Beyoncé Zaibwa Katika Tukio la Wizi Atlanta

Sangiza iyi nkuru

Polisi wa jiji la Atlanta, Marekani, wamethibitisha kuwa nyimbo ambazo hazijatolewa rasmi za mwanamuziki nyota Beyoncé zimeibwa kutoka kwenye gari la kukodi lililokuwa likitumiwa na mnenguaji wake mkuu, Christopher Grant, wakati wa Tamasha la Cowboy Carter wiki iliyopita.

Vifaa hivyo vya muziki vilivyokuwa na nyimbo hizo, video, ratiba za matamasha yaliyopita na yajayo, vilikuwa kwenye mifuko miwili iliyoibwa kutoka kwenye gari la aina ya Jeep Wagoneer, lililokuwa limeegeshwa eneo la Krog Street mnamo tarehe 8 Julai 2025.

Mnenguaji mwingine, Diandre Blue, pia ameripoti kuibiwa kompyuta yake ya MacBook Air pamoja na headphones, kwa mujibu wa taarifa ya polisi.

Bidhaa zingine zilizoibwa ni pamoja na mavazi yenye thamani ya $1,000, miwani ya Tom Ford ya $500, na vitu vingine vyenye thamani ya $750.

Polisi wametoa hati ya kukamatwa kwa mtuhumiwa mmoja, ingawa jina lake bado halijawekwa wazi.

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *