IMG-20250704-WA0001

Republican Guard Yaibuka Mabingwa wa Kombe la Ukombozi la RDF 2025

Sangiza iyi nkuru

Alhamisi hii, mashindano ya kila mwaka ya Kombe la Ukombozi la RDF 2025 yalihitimishwa kwa mafanikio, yakiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Miaka 31 ya Ukombozi wa Rwanda, kupitia michezo ya kijeshi.

Katika soka, fainali ilipigwa kwenye Uwanja wa Kigali Pele saa 10 jioni, kati ya Republican Guard (walinzi wa Rais na viongozi wakuu) na timu ya Divisheni ya 3. Mchezo ulikuwa na ushindani mkali na juhudi kubwa kutoka pande zote.

Divisheni ya 3 ilianza kwa kasi, ikionyesha pasi nzuri na mashambulizi, lakini hadi dakika ya 20, Republican Guard wakaanza kumiliki mchezo.

Dakika ya 25, Republican Guard walipata kona iliyochongwa vizuri, nahodha wao Afande Ian Kagame akaipiga kwa kichwa, lakini mpira ukapita juu ya lango.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kwa upande wa Republican Guard, wakisaka bao la ushindi. Dakika ya 47, walipata penalti iliyopigwa na Shema Mick, lakini akaukosa kwa kupiga juu ya goli.

Mchezo uliendelea hadi dakika ya 87, ambapo Republican Guard walifunga bao pekee la ushindi kupitia ushirikiano mzuri wa wachezaji. Mchezo ukaisha 1-0, na Republican Guard kutwaa taji la mwaka 2025.

Republican Guard pia walitwaa ubingwa wa Volleyball, wakionesha ubora wao katika mashindano haya ya kijeshi.

Fainali ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kijeshi na kiraia, akiwemo familia ya Afande Ian Kagame.

Jenerali Mkuu wa RDF, Gen. Mubarakh Muganga, aliwapongeza washiriki wote kwa nidhamu na ari waliyoionyesha katika mashindano hayo.

Kama sehemu ya ushirikiano wa kijeshi wa kikanda, Rwanda kwa sasa inahudumiwa na majeshi kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), wakifanya kazi za matibabu na maendeleo kwa jamii.

Miongoni mwao ni ujumbe kutoka Uganda ukiongozwa na Lt Gen. Kayanja Muhanga, Kenya na Maj Gen. Frederick Leuria, na Burundi na Brig Gen. Gaspard Baratuza, pamoja na wageni mashuhuri wengine.

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *