Leo tunarejea kwenye moja ya silaha hatari za Urusi ambazo zinaweza kuiweka dunia kwenye hatari kubwa endapo Vita vya Dunia vya Tatu vitazuka: RS-28 Sarmat. Warusi wanaiita RS-28 Sarmat, huku NATO wakiipa jina la Satan 2.
Ni moja ya makombora yenye kuogopesha duniani, yakiainishwa kama kombora zito la masafa marefu (Intercontinental Ballistic Missile – ICBM). Sarmat, au Satan 2, ni silaha ya kimkakati ya kuwatisha maadui wa Urusi.
Kombora hili lilitangazwa kwa mara ya kwanza na Rais Vladimir Putin mnamo Machi 1, 2018. Lilianza kutumika rasmi mwezi Septemba 2023.
Sifa za Satan 2:
-
Uzito: tani 208.1
-
Urefu: mita 35.3
-
Kipenyo: mita 3
-
Umbali wa kulenga: hadi km 18,000
-
Idadi ya vichwa vya nyuklia: hadi 12

Kombora hili la nyuklia lina nguvu ya uharibifu ya megatoni 50, ambayo ni mara 2,000 zaidi ya mabomu yaliyodondoshwa na Marekani huko Hiroshima na Nagasaki wakati wa Vita vya Pili vya Dunia.
Wataalamu wanasema kwamba Satan 2 inaweza kufuta nchi kama Ufaransa kwa dakika 6 tu.
Kwa mfano, ikiwa litarushwa kutoka Moscow hadi Paris (takriban km 10,000), lingefika kwa dakika 6 pekee kwa mwendo wa km 7 kwa sekunde.
Hadi sasa, hakuna mfumo wowote wa ulinzi wa makombora duniani unaoweza kulizuia kombora hili kutokana na mwendo wake wa kasi kubwa, kwa mujibu wa Kremlin walipolitangaza rasmi.
Satan 2 ni miongoni mwa silaha za kimkakati za kuzuia maadui, kama vile Kinjar, ambayo tutajadili katika makala zetu zijazo.
Katika uchambuzi ujao, tutachambua tofauti kati ya mifumo ya ulinzi dhidi ya ndege na makombora kama vile S-400 ya Urusi (iliyopendelewa na Uturuki ambaye ni mwanachama wa NATO) na mfumo wa Patriot wa Marekani.
Uchambuzi na Rudahunga Désiré


