arton102488

Trump Awaalika Kagame na Tshisekedi Washington Baada ya Makubaliano ya Amani

Sangiza iyi nkuru

Rais wa Marekani Donald Trump amewaandikia Rais Paul Kagame wa Rwanda na Rais Félix Antoine Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), akiwaalika rasmi mjini Washington.

Trump alitia saini mwaliko huo siku ya Ijumaa iliyopita, siku chache baada ya Rwanda na DRC kusaini makubaliano ya amani yaliyolenga kumaliza uhasama uliodumu kwa miongo kadhaa kati ya nchi hizo mbili.

Makubaliano hayo yalisainiwa na Mawaziri wa Mambo ya Nje: Balozi Olivier Nduhungirehe wa Rwanda na Thérèse Wagner Kayikwamba wa DRC.

Katika mwaliko wake, Rais Trump aliwashukuru viongozi hao kwa kumaliza kile alichokitaja kuwa ni “miongo mingi ya migogoro” kati ya Kigali na Kinshasa.

Iwapo hakutakuwa na mabadiliko yoyote, marais hao wawili wanatarajiwa kupokelewa katika Ikulu ya White House mjini Washington mwezi ujao (Julai). Ziara hiyo inatarajiwa kuwa njia ya kuimarisha ushirikiano kati ya Rwanda na DRC, hasa katika maendeleo ya kiuchumi.

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *