Wengi hujiuliza: “Kumaliza mapema ni nini, na kwa nini ni jambo la siri kubwa kwenye ndoa nyingi?” Ni swali linaloonekana rahisi lakini lenye uzito mkubwa. Kwa mujibu wa wataalamu wa afya ya ngono, kumaliza mapema ni pale mwanaume anapotoa mbegu kabla tendo la ndoa kuanza ipasavyo, au ndani ya dakika mbili. Ni jambo la ghafla na changamoto kubwa kwa wanandoa wengi.
Madaktari na wanandoa mbalimbali wamebaini kuwa hali hii huleta madhara kama vile:
-
Msongo wa mawazo na huzuni kwa wanaume
-
Kukosa kuridhika kwa wapenzi
-
Maugomvi na tuhuma za usaliti
Sababu za kumaliza mapema: Si mwili tu, hata akili hushiriki
Kulingana na tovuti ya afya Umuti Health, ingawa chanzo halisi hakijafahamika kwa uhakika, tafiti zinaonyesha sababu zinazochangia:
-
Kufanya mapenzi kwa mara ya kwanza au na mtu usiyemzoea
-
Kutokufanyiwa tohara, hali inayosababisha upele au msisimko mwingi
-
Hofu, wasiwasi au sononeko
-
Baadhi ya mitindo ya kufanya mapenzi huchochea kumaliza haraka
Je, inaweza kutibiwa? Ndiyo, hizi hapa njia salama na rahisi
Madaktari wa afya ya uzazi wanasema hali hii inaweza kudhibitiwa kwa msaada wa mbinu mbalimbali, mwenyewe au kwa msaada wa mwenza:
-
Jifunze kujituliza
Ukihisi uko karibu kumaliza, simama kidogo. Vuta pumzi nyingi na fikiria vitu visivyo vya ngono (kama mechi ya mpira au jambo la kuchekesha), kisha endelea. -
Bonyeza kichwa cha uume
Kwa kutumia mikono laini, mwenyewe au na mwenza, hii hupunguza msisimko. -
Fanya tendo kwa utaratibu
Epuka haraka au aibu. Chukua muda wako. Mapenzi si mashindano. -
Fikiria tohara
Utafiti fulani unaonyesha tohara hupunguza hali ya kumaliza mapema. -
Badilisha mikao ya kufanya mapenzi
Wakati mwanaume yuko chini, anaweza kujizuia kumaliza haraka. -
Tumia kondomu
Njia rahisi ya kupunguza msisimko mkali kupita kiasi.

