Wanyarwanda wameanza wiki moja ya kumbukumbu ya mauaji ya kimbali dhidi ya Watutsi mwaka 1994.
Wakati huo watu zaidi ya miliyoni moja waluawa. Jambo hili halitatokea kama mwaka uliopita kutokana na uwepo wa virusi vya Corona ambavyo vimesababisha watu kubaki nyumbani kwa ajili ya kujikinga.
Katika hotuba yake, Rais wa Rwanda, Paul Kagame amesema ni vigumu mno kwa walionusurika mauaji ya kimbari kukumbuka wakiwa nyumbani kwao. Hata hivyo, Kagame amesema haitazuia watu kukumbuka.
Ujumbe maalumu wa kila suku katika wiki hii utawasilishwa kutumia vyombo vya habari vikiwemo: Rediyo, televisheni na mitandao ya kijamii kama ilivyotangaza Tume ya Kupambana na Mauaji ya kimbari.
Isangize abandi
Tanga igitekerezo