Mahakama ya Kati ya Gasabo iliyoko Rusororo imetoa uamuzi kuhusu rufaa ya Habiyambere Zacharie, anayefahamika zaidi kama Askofu Gafaranga, na imeikataa rasmi ombi lake la kuachiliwa.
Askofu Gafaranga ataendelea kushikiliwa mahabusu akisubiri kesi yake ya msingi juu ya tuhuma za kupiga, kujeruhi, na kumnyanyasa mkewe, Annet Murava.
Mahakama ilibaini kuwa sababu alizotoa kwenye rufaa hazikuwa na msingi wowote, na hakuna ushahidi wa ukiukaji wa haki zake katika uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Mwanzo ya Nyamata iliyomweka mahabusu kwa muda tangu Mei 23, 2025.
Katika kikao kilichofanyika Julai 7, 2025, Askofu Gafaranga hakuwahi kuomba msamaha, wala kuonyesha majuto yoyote. Badala yake, alikanusha tuhuma na kudai kuwa anabughudhiwa kimakusudi na upande wa mashtaka.
Alikamatwa na Rwanda Investigation Bureau (RIB) tarehe 7 Mei 2025 kufuatia malalamiko yaliyowasilishwa na mkewe.


