20250530_142129

Kabila Arejea Goma na Kukutana na Viongozi wa Jadi wa Kivu Kaskazini

Sangiza iyi nkuru

Joseph Kabila Kabange, aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, siku ya Ijumaa alikutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa jadi kutoka mkoa wa Kivu Kaskazini.

Kabila amekuwa Goma tangu Jumapili iliyopita. Amerudi nchini baada ya kuwa uhamishoni kwa muda mrefu tangu mwaka 2023.

Alikutana na viongozi hao wa jadi, siku moja baada ya kuwapokea viongozi wa kidini wanaofanya kazi katika Kivu Kaskazini.

Habari pia zinaeleza kuwa wiki hii Joseph Kabila amekutana na wanasiasa mbalimbali, akiwemo Corneille Nangaa, mratibu wa Muungano wa Mto Kongo (Alliance Fleuve Congo) ambao unajumuisha kundi la M23.

Ripoti zinaonyesha kuwa Kabila anaendelea na mashauriano na watu wa kada mbalimbali ili kutafuta suluhisho la pamoja kwa ajili ya kuisaidia DRC kutoka kwenye matatizo yanayoikabili, ambayo yamechochea vita dhidi ya waasi wa M23 kwa zaidi ya miaka mitatu sasa.

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *