Bwiza
ads

Kigali: Mashabiki wampiga mchezaji kwa shutuma za ulozi

Habari Mpya•
Fred Rugira
By Fred Rugira
•Kuwa Gatatu, 4 Ukuboza 2019 saa 16:00
Iminota 1 yo gusoma
Kigali: Mashabiki wampiga mchezaji kwa shutuma za ulozi

Mashabiki wa Timu ya APR wawili wamekamatwa na kufungwa juu ya kumpia mchezaji wa Timu ya Gicumbi FC, Mghana, Vanderpuije Daniel.

Wawili walimpiga jana tarehe3 Disemba baada ya kutoka sare kati ya timu hizo mbili.

Ofisi ya Uendeshamashtaka nchini Rwanda, RIB, imetangaza kumeanzishwa upelelezi kuhusu kisa hicho na watuhumiwa ambao hawakutajwa majina watasimama kizimbani watakapoonekana kuwa na hatia.

Hata hivyo, hakuna tangazo lolote lililotloewa na Timu ya APR kukema jambo la mashabiki wa timu hiyo ya jeshi.

Fred Rugira

Inkuru yanditswe na: Fred Rugira

Umunyamakuru wa BWIZA.COM wanditse inkuru 4,448.