Kigali: Wakazi watokwa na machozi kwa kubomolewa nyumba na serikali

Sangiza iyi nkuru

Wakazi maeneo mbali mbali Mjini Kigali wametokwa machozi katika wikendi ambako viongozi walitoa amri nyumba zao zibomolewe kutokana na kuishi mahali ambako ni hatali kwa maisha yao.

Hilo limetokea maeneo yakiwemo Gatsata, Kiruhura, Rwampara, Kacyiru na kwingine.

Wananchi wamesema waliamuriwa kutoka nje kwa ghafla na mali zao zikaharibika.

Wakazi eneo la Gatsata, wamesema wana hati miliki za ardhi yao lakini wanabomolewa nyumba.

Viongozi Mjini Kigali wamesema lazima wakazi hao wahamaie mahali kwingine ambako maisha hayamo hatarini wakati huu wa mvua nyingi.

Wakazi wamesema hawana mahali pa kwenda na wanataka wapatiwe fidia ya ardhi na nyumba zao.

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *