20250514_111301

Madaktari wa DRC Watishia Kuhamia Rwanda kwa Sababu ya Mishahara

Sangiza iyi nkuru

Madaktari katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wameionya serikali kwamba wanaweza kuhamia Rwanda endapo hawatalipwa malimbikizo ya mishahara wanayodaiwa.

Madaktari hao walitoa onyo hilo Jumatano tarehe 13 Mei, wakati wa maandamano ya kudai malipo yao kutoka kwa serikali.

Maandamano hayo yalifanyika mjini Kinshasa, mji mkuu wa nchi hiyo.

Katika video zinazozagaa mitandaoni, madaktari hao wanasikika wakiimba nyimbo zenye ujumbe unaoelekezwa kwa serikali: “Kama hamtaki kutulipa, tunaenda Rwanda. Tumechoka na Congo.”

Walikuwa pia wamebeba mabango yenye ujumbe unaoitaka serikali ya DRC kuwalipa mishahara na marupurupu yao mara moja.

Malimbikizo ya mishahara wanayodai ni tangu mwezi Januari mwaka huu.

Wafanyakazi hawa wa afya wanalalamikia njaa, huku Rais Félix Antoine Tshisekedi akiwa ametangaza hivi karibuni kuongeza mishahara ya madaktari na watumishi wengine wa serikali, akiwemo wanajeshi.

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *