Bwiza

Majengo matano yamefungwa kwa ajili ya usalama Mjini Kigali

Habari Mpya•
Fred Rugira
By Fred Rugira
•Kuwa Gatanu, 30 Ukwakira 2026 saa 15:21
Majengo matano yamefungwa kwa ajili ya usalama Mjini Kigali

Jiji la Kigali limeamuru kufungwa kwa muda kwa majengo matano kutokana na kushindwa kutimiza viwango vya usalama dhidi ya moto.

Kufungwa huko, kunakoanza Jumamosi, Oktoba 31, kunalenga kushughulikia masuala ya usalama yanayotokana na kutokuzingatia masharti ya usalama dhidi ya moto, kwa mujibu wa taarifa ya jiji iliyotolewa Ijumaa.

Majengo yaliyoathiriwa ni Agakiriro iliyoko Kabuga, jengo la Umukindo na Comejoga zilizoko Gisozi, ASMMS Ltd iliyoko Kicukiro, pamoja na Soko la Gahoromani.

Jiji lilisema majengo hayo yanafungwa kwa “kushindwa kuzingatia masharti ya usalama dhidi ya moto, jambo linaloweka maisha ya watu na mali zao hatarini.”

“Wamiliki wa majengo hawapaswi kuwatoza wapangaji kodi kwa kipindi ambacho majengo hayo yatakuwa yamefungwa,” ilisema taarifa ya jiji.

Wapangaji wenye bidhaa zinazoharibika haraka au vitu vingine vinavyohitaji kuondolewa haraka wametakiwa kuviondoa kabla ya kufungwa kwa majengo hayo, kutakakoanza kutekelezwa Jumamosi jioni.

Jiji limewataka wamiliki na wasimamizi wa majengo hayo kuchukua hatua za kurekebisha kasoro zilizobainika, likisisitiza kuwa wanapaswa kufanya hivyo “bila kuchelewa ili kuhakikisha usalama wa umma na kuwezesha shughuli za biashara kurejea katika hali ya kawaida haraka iwezekanavyo.

Hatua hii inafuatia mfululizo wa matukio ya moto yaliyotokea mu karibuni jijini Kigali, ikiwemo moto ulioteketeza jengo lenye baa ya Sport Light Lounge iliyoko Kabeza, Jumapili, Oktoba 25, na mwingine uliotokea katika Kituo cha Biashara cha Gisozi, na kusababisha uharibifu katika maeneo kadhaa ya biashara.

Pia, inafuatia moto ulioteketeza GIOCO Plaza, soko kubwa zaidi katika Wilaya ya Musanze, Oktoba 10. Baada ya tukio hilo, wafanyabiashara walieleza wasiwasi wao kuhusu msongamano wa watu, uhaba wa maji, upatikanaji mdogo wa vifaa vya kuzimia moto ndetse na vifaa vya usalama dhidi ya moto vilivyokuwa vimepitwa na muda wa matumizi.

Fred Rugira

Inkuru yanditswe na: Fred Rugira

Umunyamakuru wa BWIZA.COM wanditse inkuru 4,448.