sud_kivu_pluie_torrentielle_a_kasaza_11_mai_2025_jpg_711_473_1

Mvua Kali Yaua Watu 100+ Fizi, Yabomoa Nyumba 150 na Kuwacha Mamia Bila Makaazi

Sangiza iyi nkuru

Kijiji cha Kasaza katika Wilaya ya Fizi (Kivu Kusini) kilikumbwa na mvua kubwa isiyo ya kawaida usiku wa Alhamisi, tarehe 8 hadi Ijumaa, tarehe 9 Mei 2025, na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 100.

Idadi ya waliokufa na uharibifu inaendelea kuongezeka. Kwa mujibu wa kiongozi wa Wilaya, Samy Kalonji, miili zaidi ya 110 imepatikana, watu zaidi ya 40 wamejeruhiwa, nyumba 150 zimebomolewa, na watu 850 hawana tena makazi.

Kama ilivyoripotiwa na mediacongo.net, juhudi za uokoaji zinaendelea kwa mikono bila vifaa, hali inayozua hofu kuwa idadi ya vifo huenda ikaongezeka zaidi.

Katika kukabiliana na janga hili, Samy Kalonji alitoa wito wa msaada:

“Tunaomba serikali ya kitaifa na ile ya jimbo kutusaidia kuwasitiri ndugu zetu waliopoteza maisha kwa heshima. Miili mingi bado iko chini. Tunahitaji majeneza na msaada wa maziko ya heshima.”

Aidha, ametoa wito kwa mashirika ya kibinadamu kuingilia kati, kwani familia nyingi hulala nje bila makazi, chakula wala huduma za afya.

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *