Rais wa Urusi, Vladimir Putin, ametoa pendekezo la kuanzisha mazungumzo ya moja kwa moja na Ukraine.
Akizungumza na waandishi wa habari asubuhi ya Jumapili, Putin alisema kuwa mazungumzo hayo yanapaswa kulenga kuleta amani ya kudumu na kuondoa chanzo kikuu cha vita.
“Tunawaomba viongozi wa Kyiv kurejelea mazungumzo ya amani siku ya Alhamisi [tarehe 15 Mei] huko Istanbul,” alisema Putin.
Kwa mujibu wa Deutsche Welle, aliongeza: “Wanaotaka amani ya kweli hawawezi kukataa pendekezo hili.”
Putin pia alisema atazungumza na Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan.
Mojawapo ya sababu kuu alizozitaja Putin kama kichocheo cha vita ambavyo sasa vina miaka mitatu, ni juhudi za NATO kupanuka hadi kwenye mipaka ya Urusi kwa kuishawishi Ukraine kujiunga. Anasema kuwa Ukraine kama ingesitisha mpango huo, mgogoro ungeisha, lakini rais mwenzake, Zelenskyy, alikataa.


