Mshambuliaji wa APR FC, Denis Omedi, ametunukiwa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka kwenye Ligi Kuu ya Uganda baada ya kuonyesha kiwango cha juu akiwa na Kitara FC, kabla ya kujiunga na Rwanda.
Shirikisho la Soka la Uganda (FUFA) limemzawadia gari jipya pamoja na shilingi milioni moja za Uganda.
Mbali na kuwa Mchezaji Bora wa Mwaka, Omedi alipiga bao bora zaidi la msimu na pia akaingia katika kikosi bora cha mwaka. Alikuwa anawania tuzo hiyo na wachezaji nyota kama Ssekiganda Ronald na Allan Okello.
Omedi pia ameitwa kwenye timu ya taifa ya Uganda, itakayocheza mechi za kirafiki dhidi ya Cameroon na Gambia mwezi Juni 2025.



