Klabu ya Azam FC kutoka Tanzania ipo kwenye mazungumzo ya kumsajili mshambuliaji Mamadou Sy anayekipiga kwa sasa katika timu ya APR FC ya Rwanda.
Mchezaji huyu mwenye umri wa miaka 24 kutoka Mauritania tayari amecheza mechi 6 katika Ligi Kuu ya Rwanda msimu huu, akiwa amefunga mabao 4.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Africa Transfer Market, Azam FC imeshaonyesha nia ya kumsajili straika huyo, ambapo inadaiwa anaweza kusajiliwa kwa pauni 100,000 — sawa na takriban milioni 153 za fedha za Rwanda.
Mamadou Sy ameendelea kuonyesha uwezo mkubwa katika ligi ya Rwanda, jambo lililowavutia vilabu vikubwa vya ukanda huu wa Afrika Mashariki.
Bado inasubiriwa kuona kama mazungumzo kati ya APR FC na Azam FC yatafanikiwa, na kumfanya Mamadou Sy kuelekea Dar es Salaam.


