Msanii wa Uganda Weasel Manizo amefichua kuwa katika safari yake ya muziki aliwahi kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na wanawake wakubwa — maarufu kama “sugar mummies” — lakini sasa ameacha kabisa.
Akihojiwa na vyombo vya habari, Weasel alisema kuwa mahusiano hayo yalimsadia sana katika nyakati ngumu za maisha yake ya kisanii, lakini kwa sasa yuko kwenye uhusiano wa upendo na mke wake Sandra Teta.
Alisema:
“Niliwahi kufanya hivyo, lakini niliacha. Hilo nimeliachia wasanii wengine.”
Alikataa kuwataja wale ambao bado wanaendelea na maisha hayo, lakini alikiri kuwa ni jambo linaloendelea katika tasnia ya burudani.
Kauli yake inakuja baada ya msanii mwingine, Grenade Official, naye kukiri kuwa huwa anadate na wanawake wakubwa kwa sababu wanampenda kutokana na sura na mvuto wake.


