682442a6b45b2a001d56eeb3

Wema Sepetu Azungumza Baada ya Uvumi wa Kifo—‘Mimi Bado Nipo Hai!’

Sangiza iyi nkuru

Mwigizaji maarufu na aliyewahi kuwa Miss Tanzania, Wema Sepetu, ameibuka na kukanusha uvumi wa kifo chake uliosambaa mitandaoni kupitia picha iliyomuonesha kama aliyefariki dunia.

Picha hiyo, ambayo ilionekana kama taarifa ya dharura kutoka kwenye televisheni ya Millard Ayo, ilisomeka:
“Wema Sepetu amefariki dunia.”

Hata hivyo, Wema mwenyewe alijitokeza kwa sauti na video, akithibitisha kuwa yuko hai, na kulaani vikali aliyeeneza taarifa hizo za uongo.

Akasema:

“Wanasema nimekufa? Na bado nazungumza? Aliyefanya haya, Mungu anakutazama. Haya ni uongo, na yanawaumiza wanaonipenda.”

Mashabiki wake waliingiwa na mshtuko mkubwa, wengine wakiyaita matusi ya wazi, na baadhi wakisema walipatwa na hofu kali.

Nyota huyo anayependwa Afrika Mashariki alionya kuwa kuchezea masuala ya kifo si jambo la mzaha, na akatoa wito kwa watu wathamini maisha na wasimame kwa ukweli, badala ya kusababisha huzuni kwa habari za uongo.

Soma Izindi Nkuru

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *