Mwanamume mwenye umri wa miaka 20 kutoka Uganda anaweza kukabiliwa na hukumu ya kifo baada ya kushtakiwa kwa ulawiti uliokithiri, ambao ni kosa la kifo chini ya sheria tata ambayo ilipitishwa mwezi Mei.
Ni mara ya kwanza kwa shtaka kama hilo kuripotiwa, ingawa haijulikani wazi ikiwa kumekuwa na mashtaka yoyote hapo awali.
Mahakama moja mashariki mwa Uganda ilimfungulia mashtaka mwanamume huyo tarehe 18 Agosti, kufuatia madai kwamba alijihusisha kimapenzi na mwanamume mwenye umri wa miaka 41.
Lakini haikuwa wazi kwa nini ilizingatiwa kuwa hii ilikuwa chini ya kitengo cha "ushoga uliokithiri", shirika la habari la Reuters linaripoti.
Kwa mujibu wa sheria, kundi la "waliokithiri" ni pamoja na kufanya mapenzi ya jinsia moja na mtu aliye chini ya umri wa miaka 18 au pale mtu anapoambukizwa ugonjwa wa maisha ukiwemo HIV au VVU.
Justine Balya, wakili wa mshtakiwa, aliiambia Reuters kwamba Uganda imewafungulia mashtaka watu wengine wanne chini ya sheria yake ya kupinga ushoga lakini mteja wake ndiye wa kwanza kufunguliwa mashtaka chini ya aina hii ya adhabu.
Tarehe 22 Agosti, mahakama ya Uganda ilimshtaki mwanaharakati wa zamani wa haki za mashoga na mwanamume mwingine kwa ulawiti, kulingana na gazeti la Daily Monitor la Uganda.
Wiki iliyopita, mahakama nyingine ya Uganda ilimshtaki mwanamke mwenye umri wa miaka 26 kwa ulanguzi wa binadamu na makosa matatu ya ulawiti.
Mapema mwezi huu, Benki ya Dunia ilisema inasitisha mikopo mipya kwa Uganda kwa sababu sheria ya kupinga ushoga inakinzana na maadili yake ya msingi.
Tanga igitekerezo