Mmoja mwa maafisa wa Polisi kwenye kituo chao cha Byumba, Wilayani Gicumbi amepiga risasi na kumuua mfungwa kwa majina ya Wellars Igirukwayo,42.
Taarifa ni kwamba mfungwa alikuwa amefungiwa kwenye kituo cha polisi alijaribu kutoroka.
Haijaeleweka waziwazi namna ambavyo mfungwa alikuwa kwenye kituo cha polisi badala ya kuwa gerezani.
Msemaji wa Polisi Mkoa wa Kaskazini, CIP Alex Rugigana amehakikisha taarifa hizo.
Wellars alikuwa gerezani kwa shutuma za mpango wa kumuua mkewe.
Isangize abandi
Tanga igitekerezo