Mtume kwa majina ya Liliane Mukabadege amekamatwa jana na jeshi la polisi Mjini Kigali juu ya uongo wa anapokwenda wakati wa kujikinga virus vya Corona.
Mukabadege anadaiwa kuwadanganya polisi kuwa anakwenda mjini kwenye show ya radio lakini akachepuka kuelekea kanisani.
" Jeshi la polisi limekamata mtume Mukabadege kwa kudanganya kuwa anakwenda kwenye radio. Polisi imemfuata na kugundua kuwa anaelekea kanisani eneo la Kimisagara." Polisi imesema
"Gari lake pia limekataifishwa" Polisi imeongeza
Jeshi la Polisi limeonya watu waache kudanganya na kuwa mwenye hatia atakamatwa halafu apatiwe adhabu.
Pamoja na hayo, Rwanda ina wagonjwa wa virus vya Corona 100. Serikali imeendelea kutilia mkazo mikakati ya kujikinga ugonjwa huu.
Isangize abandi
Tanga igitekerezo