Rais Paul Kagame wa Rwanda alisema hadharani kuwa anataka mwanamke ashike mikoba yake.
Alisema hilo jana wakati wa mkutano wa Mushikirano mjini Kigali.
" Muongeze mwondo, sijui wanavyodhani wanaume lakini nafasi hii nigenpenda ichukuliwe na mwanamke." alisema Kagame
Kwa sasa wengi wanajiuliza miongoni mwa wanawake nani anaweza kuwa Rais wa Rwanda.
Baadhi ya wanaotajwa ni mkewe Rais Kagame, bintiye Kagame, Ange Ingabire Kagame, Katibu Mkuu wa OIF, Louise Mushikiwabo n.k
Inatarajia kuwa akiwa na nia, Kagame ataondoka madarakani mwaka 2034.
Hata hivyo, alipokuwa nchini Qatar alisema inawezekana hataendelea kutawala Rwwanda baada ya mwaka 2024.
Isangize abandi
Tanga igitekerezo