Ofisi kuu ya Uchunguzi wa Uhalifu nchini Rwanda (RIB) imepiga marufuku taarifa kwamba raia ya Uingereza, Mathew Robert alifariki kutokana na Coronavirus.
Msemaji wa RIB, Marie Michelle Umuhoza ameambi vyombo vya habari nchini kuwa walifanya uchunguzi kwa mwili wa marehemu halafu wakaona kuwa kifo hakikusababishwa na COVID-19 kama ilivyozagaa kwenye mitandao ya kijamii hasa Twitter
Anayewakilisha Uingereza nchini Rwanda, Jo Lomas amesema familia ya marehemu iliwasiliana na serikali ya Rwanda kuhusu jambo hili.
RIB wametangaza familia ina ruhusa kutangaza matokeo ya waganga husika na kifo cha Robert.
Kwa sasa, Rwanda haijatangaza kifo cha mtu juu ya COVID-19.
Isangize abandi
Tanga igitekerezo