Wakazi wa kisiwa cha Nkombo Wilayani Rusizi, Kusini Magharibi mwa Rwanda wamesema kuna hofu ya kuuawa na njaa juu ya Virus vya Corona.
Wametangaza kuwa wanatii amri ya serikali ya kubaki nyumbani lakini wanaweza kuuawa na nja kutokana na kutokuwa na chakula.
Wanaitaka serikali kuwasaidia hasa chakula kwani kazi walizokuwa wakifanya zilikomeshwa hadi tarehe 19 Aprili mwaka huu.
Jean de Dieu Tuyishime, Katibu Mtendaji wa Tarafa ya Nkombo amesema yeyote anayetaka kwenda kununua chakula nje ya kisiwa anapatiwa rukhusa.
Wakazi 19,000 wanaishi Kisiwani Nkombo na 80% ni wavuvi.
Isangize abandi
Tanga igitekerezo